Daktari wa China aombolezwa nchini Tanzania kwa kujitoa maisha kishujaa (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 23, 2025
Daktari wa China aombolezwa nchini Tanzania kwa kujitoa maisha kishujaa
Zhang Junqiao (kulia) akimwokoa mwanamke aliyekuwa anazama kwenye ufukwe wa Dar es Salaam, Tanzania, Juni 15, 2025. (Xinhua)

DAR ES SALAAM - "Bila kujali utaifa au rangi, ninachothamini zaidi ni uhai," Zhang Junqiao, daktari wa usingizi na ganzi wa China, aliwahi kusema hayo. Mwishoni mwa wiki siku ya Ijumaa asubuhi, watu zaidi ya 300 walikusanyika kwa ukimya mzito kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, Tanzania, wakiwa wamesimama bega kwa bega kumuaga Zhang, kiongozi wa kundi la 27 la timu ya madaktari wa China nchini humo ambaye amepoteza maisha wakati akimwokoa mtu aliyekuwa akizama.

Hafla ya kumuaga, iliyofanyika kwa heshima kubwa na mioyo mizito, ilitoa heshima kwa Zhang, ambaye picha yake ilikuwa imezungukwa na maua meupe. Wengi walikuwa wamevalia mashati meupe yaliyonakshiwa kwa uso wake wenye tabasamu, huku wengine wakiinua fulana iliyofunikwa kwa majina yaliyoandikwa kwa mkono -- ishara za shukrani na huzuni. Waombolezaji wenye machozi walikuwa wakinong'ona jina lake. "Alikuwa ni Mchina. Lakini kwetu, alikuwa familia kila wakati” muuguzi mmoja amesema.

Zhang alifariki Juni 15, Siku ya Akina Baba Duniani, wakati akimwokoa mwanamke aliyekuwa akizama kwenye pwani ya Dar es Salaam. Picha za mashuhuda zinamuonyesha akiwa amemshika juu ya maji na kumsaidia kumvisha jaketi la kuokoa maisha kabla ya kutoweka chini ya mawimbi. Licha ya juhudi za wenzake kumuokoa, Zhang hakuweza kuamka.

Zhang, mwenye umri wa miaka 38, alikuwa nchini Tanzania kutoka Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China na alikuwa amepangiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kituo kikuu cha rufaa nchini humo, tangu mapema mwaka 2024.

Akiwa daktari mwandamizi mtaalamu wa ganzi, alibadilika haraka kuendana na mahitaji ya dharura ya hospitali hiyo, ambapo madaktari wachache sana hawafiki 20 wanahudumia kituo kinachoendesha vyumba saba hadi vinane vya upasuaji.

Badala ya kujiwekea kikomo kwa kazi ya kliniki pekee, Zhang alijikita katika kujenga uwezo. "Lazima nifundishe. Lazima nibaki kitu hapa," Zhang aliwaambia wenzake.

Kweli kwa neno lake, Zhang alianzisha programu za mafunzo kwa vitendo kwa wafanyakazi na wanafunzi wa matibabu wenyeji. Alianzisha mbinu za hali ya juu kama vile vizuizi vya neva vinavyoongozwa na ultrasound kwa kutumia mifano ya kuiga, ya kwanza katika mafunzo ya wenyeji. Akifanya kazi na Jumuiya ya Wauguzi Wataalam wa Ganzi Waliosajiliwa Tanzania, madarasa yake yalipongezwa kwa thamani yake ya kivitendo.

"Aliniongoza kwa utulivu wakati nikifanya intubation. Si tu alinifundisha jinsi ya kuifanya. Alinifanya niamini kuwa ninaweza" amekumbushia Elick Mwakatungila, muuguzi kijana mtaalam wa ganzi.

"Tumepoteza daktari wa kweli. Ameokoa mtu mwingine kwa mikono yake. Hakuwa wa nchi yetu, lakini ametoa maisha yake kwa ajili ya watu wetu." mtanzania mmoja ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii. Maoni mengine yanasomeka: "Tumempoteza daktari bingwa,"

Ujumbe wa mwisho kwenye mtandao wa kijamii wa Zhang ulibeba dhamira yake: "Kuhudumia watu hakujui mipaka. Kama daktari wa China, ninajivunia kuwezesha wenzangu wa Tanzania kuhisi nguvu ya nchi yetu na taaluma yetu." 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha