Bustani ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang, China: Utambulisho Mpya wa Michezo Mjini (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 24, 2025
Bustani ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang, China: Utambulisho Mpya wa Michezo Mjini
Vijana wakifanya mazoezi ya kuendesha baiskeli kwenye njia ya miinuko na mabonde, pump track. (Picha na Zhang Lulu/Peoples’ Daily Online)

Katika eneo la urithi wa kiviwanda mjini Shenyang, Mkoa wa Liaoning, China, mfumo wa chuma chenye kutu na njia za mbio za baiskeli zenye rangi mbalimbali kwa pamoja huunda muundo mpya alama kwa mji huo wenye historia ndefu — Bustani ya Kimataifa ya Njia za Miinuko na Mabonde za Baiskeli (Pump Track) ya Shenyang.

Ikiwa ni eneo la kwanza la njia za miinuko na mabonde kwa michezo ya baiskeli kaskazini-mashariki mwa China kupata ithibati kutoka Shirikisho la Kimataifa la Michezo ya Kuendesha Baiskeli (UCI), eneo lake lenye ukubwa wa mita za mraba 45,800 lina aina tisa za njia hizo za mbio ili kukidhi mahitaji ya wachezaji kutoka viwango vya wanaoanza hadi wataalamu.

Ikiwa ni sehemu ya mradi wa kukarabati eneo kongwe la viwanda katika Eneo la Tiexi, eneo la awali la bustani hiyo lilikuwa eneo la kiwanda kilichoachwa bila kutumika. Timu ya wasanifu ilibakisha baadhi ya mabaki ya viwanda, na kugeuza fremu za chuma kuwa uzio wa njia hizo za mbio. Sehemu ya maonesho ya urithi wa kiviwanda imewekwa karibu na njia za mbio hizo kusimulia historia ya tasnia ya viwanda ya Shenyang.

Hadi sasa, Bustani hiyo ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang imeshakuwa mwenyeji wa mashindano mengi ya kimataifa, yakiwemo Mchujo wa Mashindano ya Dunia ya Pump Track ya UCI mwaka 2023, Mashindano ya China ya Pump Track (Shenyang) mwaka 2024, pamoja na Mchujo wa China wa Mashindano ya Dunia ya Pump Track ya Velosolutions UCI mwaka 2025.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha