Maonyesho ya Kilimo ya Rwanda yaangazia uvumbuzi kwa mifumo endelevu ya kilimo cha chakula (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 24, 2025
Maonyesho ya Kilimo ya Rwanda yaangazia uvumbuzi kwa mifumo endelevu ya kilimo cha chakula
Wakulima wakionesha aina mbalimbali za viazi mviringo chotara kwenye Maonyesho ya 18 ya Kilimo ya Kitaifa mjini Kigali, Rwanda, Juni 21, 2025. (Picha na Cyril Ndegeya/Xinhua)

KIGALI - Wakulima wa Rwanda wanaonyesha aina mbalimbali za uvumbuzi unaoleta mabadiliko katika kilimo nchini humo katika Maonyesho ya 18 ya Kilimo ya Kitaifa ya Rwanda yanayoendelea huko Kigali, mji mkuu wa nchi hiyo, maonesho hayo yanayofanyika kuanzia Juni 18 hadi 27 yamevutia waonyeshaji wapatao 500, Wizara ya Kilimo ya Rwanda imesema katika taarifa yake jana Jumatatu.

Kuanzia mifumo ya kisasa ya umwagiliaji na aina za mazao za kuzalisha kwa wingi hadi mashine za kisasa, zana bora za kilimo na mipango ya kukabiliana na tabianchi kwa teknolojia ya AI, watembeleaji wa maonyesho hayo wanaweza kuona mipango halisi ya kilimo, mipango hiyo imejaribiwa, kuthibitishwa, na tayari kutumika.

Pia vitu vinavyooneshwa ni pamoja na matrekta, mashine za kupanda mbegu kwa usahihi, mashine za kuvuna, na mashine nyingine za kuvutia zinazoonyesha jinsi matumizi ya mashine yanavyoleta mabadiliko katika kilimo nchini Rwanda.

Fredy Karegeya, mkuu wa kitengo cha uzalishaji mbegu katika kampuni ya nchini humo amesema kuwa matumizi ya mifumo ya teknolojia ya kisasa na uvumbuzi yamewezesha uzalishaji wao wa mbegu kustawi na kuleta matokeo halisi katika mifumo ya chakula nchini humo.

"Tunapanda mimea ya mazao matatu ya mahindi, maharage na soya, uzalishaji zaidi ni mahindi. Katika uzalishaji wa mbegu za mahindi, tuna aina karibu nne na nyingine ziko mbioni kuja mara baada ya majaribio ya ufanisi. Moja ya aina ya mahindi tuliyoendeleza inafaa kwenye ardhi yenye ukavu, aina hiyo ya mbegu ambayo hutoa mavuno mengi kuanzia tani tisa hadi tani 12 kwa hekta moja," Karegeya ameliambia shirika la habari la China, Xinhua kwenye mahojiano ya hivi karibuni.

Awali, Waziri wa Kilimo na Rasilimali Wanyama wa Rwanda Mark Cyubahiro Bagabe alisema maonyesho hayo ya kila mwaka yanatoa jukwaa la kuonyesha teknolojia, uzoefu wa kufanya uvumbuzi, na ushirikiano unaoshughulikia changamoto katika kilimo kuanzia mabadiliko ya tabianchi hadi hasara za baada ya mavuno. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha