Timu ya madaktari wa China yatoa msaada wa zana za matibabu kwa hospitali ya Ethiopia (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 04, 2025
Timu ya madaktari wa China yatoa msaada wa zana za matibabu kwa hospitali ya Ethiopia
Watu wakipakua zana za matibabu kutoka kwenye lori katika Hospitali ya Tirunesh-Beijing, katika kitongoji cha Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 2 Julai 2025. (Xinhua/Michael Tewelde)

ADDIS ABABA - Timu ya 25 ya madaktari wa China nchini Ethiopia imetoa msaada wa zana za matibabu zinazohitajika sana kwa Hospitali ya Tirunesh-Beijing, inayojulikana pia kwa jina la Hospitali ya Urafiki wa Ethiopia na China, iliyoko katika kitongoji cha Addis Ababa, mji mkuu wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Akihutubia hafla ya makabidhiano ya zana hizo juzi Jumatano jioni, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Tirunesh-Beijing, Eshetu Tadele, amezipongeza timu za madaktari za China za awamu mbalimbali kwa "mchango uliotolewa nao kwa kuokoa maisha" kwa watu wa Ethiopia na kwa kutoa maarifa na ujuzi wa matibabu kwa wenzao wa Ethiopia katika wakati wa kutoa huduma huko.

Amesema timu ya madaktari wa China inayotoa huduma katika hospitali hiyo imeonyesha kuwa "mfumo wa afya hauna mipaka. Ndiyo maana mmeonyesha moyo wenu na wema wenu katika kuisaidia Ethiopia."

Alisema kuwa, msaada huo mpya wa zana za matibabu ni wa mara ya tatu kutolewa kwa hospitali hiyo ndani ya mwaka mmoja, Tadele amesema msaada kama huo wa hivi karibuni, pamoja na mpango uliofanikiwa wa kuhamisha teknolojia, vimewezesha kuanzishwa kwa kitengo cha matibabu ya macho chenye zana na vifaa kamili katika hospitali hiyo.

Wakati wa kulikaribisha timu ya 26 ya madaktari wa China, jumuiya ya hospitali pia imewapongeza madaktari wa timu iliyomaliza muda wake kwa "uungaji mkono wao muhimu" katika kulinda afya na ustawi wa watu wa Ethiopia.

Imesisitiza kuwa huduma ya madaktari wa China ni udhihirisho wazi wa kuongezeka kwa mawasiliano kati ya raia wa nchi hizo mbili.

Liu Junying, mkuu wa timu ya 25 ya madaktari wa China, amesema timu yake, ambayo ilianza kazi katika Hospitali ya Tirunesh-Beijing Mei 2024, huduma za matibabu zinazotolewa kwa jamii za Ethiopia ni sehemu moja ya ushirikiano wa muda mrefu wa afya kati ya China na Ethiopia.

Timu ya 26 ya madaktari wa China iliyotumwa hivi karibuni, imeundwa na wataalam 16 wa matibabu mbalimbali, itaendelea kutekeleza jukumu la matibabu la China nchini Ethiopia, ambalo limekuwa likihudumia wakazi wenyeji tangu miaka ya 1970. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha