Rais Xi atoa heshima kwa wahanga wa kampeni ya rejimenti 105 kupigana na wavamizi wa Japan (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 08, 2025
Rais Xi atoa heshima kwa wahanga wa kampeni ya rejimenti 105 kupigana na wavamizi wa Japan
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akizungumza na wanafunzi na wafanyakazi kwenye jumba la makumbusho la kampeni ya rejimenti 105 ya kupigana na wavamizi wa Japan, wakati alipofanya ziara ya kukagua Mji wa Yangquan, Mkoa wa Shanxi, kaskazini mwa China, Julai 7, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

YANGQUAN, Shanxi - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), alitoa heshima kwa wanajeshi waliojitolea mihanga katika kampeni ya rejimenti 105 ya kupigana na wavamizi wa Japan, wakati alipofanya ziara ya kufanya ukaguzi katika Mji wa Yangquan katika Mkoa wa Shanxi, kaskazini mwa China jana Jumatatu.

Akiwa kwenye uwanja wa kumbukumbu wa kuwakumbuka wahanga wa Kampeni ya Rejimenti 105 ya kupigana na wavamizi wa Japan, Rais Xi aliweka kikapu cha maua kwa heshima ya wahanga, kisha akatembelea jumba la makumbusho la kampeni hiyo kuu.

Katika ziara hiyo, Rais Xi alifanya mapitio ya historia ya chama cha CPC kuongoza jeshi na raia katika mapambano hayo ya kijasiri dhidi ya wavamizi wa Japan, na kufahamishwa kuhusu juhudi za sehemu hiyo za kuanzisha elimu ya historia ya mapinduzi na kurithisha na kuenzi moyo mkuu wa kupambana na uvamizi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha