Jumuiya ya Kimataifa ya Utafiti wa Anga ya Kina Kirefu yaanzishwa Hefei, China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 08, 2025
Jumuiya ya Kimataifa ya Utafiti wa Anga ya Kina Kirefu yaanzishwa Hefei, China
Picha hii iliyopigwa Julai 7, 2025 ikionyesha mwonekano wa nje wa Maabara ya Utafiti wa Anga ya Kina Kirefu mjini Hefei, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China. (Xinhua/Zhou Mu)

HEFEI - Jumuiya ya Kimataifa ya Utafiti wa Anga ya Kina Kirefeu, ambayo ni jumuiya ya taaluma ya kimataifa ya kujikita katika utafiti wa anga ya kina kirefu imeanzishwa rasmi jana Jumatatu mjini Hefei, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China.

Jumuiya hiyo imeanzishwa kwa pendekezo la pamoja la Maabara ya Utafiti wa Anga ya Kina Kirefu, Kituo cha Utafiti wa Mwezi na Programu ya Anga ya Juu cha Idara ya Kitaifa ya Anga ya Juu ya China, Jumuiya ya Wanaanga wa China, Jumuiya ya Utafiti wa Anga ya Juu ya China na Mpango wa Ufaransa wa "Planetary Exploration, Horizon 2061."

Kuanzishwa kwa jumuiya hiyo pia kumefadhiliwa kwa pamoja na wanataaluma 20 kutoka China na wanasayansi 31 wa kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha