Kituo cha umeme wa jua chazinduliwa katika taasisi ya ufundi wa kazi iliyojengwa kwa msaada wa China nchini Rwanda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 10, 2025

Wanafunzi wakiendesha kifaa cha kuigilizia katika Taasisi ya Forever TVET iliyojengwa kwa msaada wa China  huko Kigali, Rwanda, tarehe 8 Julai 2025. (Picha na Huang Wanqing/Xinhua)

Wanafunzi wakiendesha kifaa cha kuigilizia katika Taasisi ya Forever TVET iliyojengwa kwa msaada wa China huko Kigali, Rwanda, tarehe 8 Julai 2025. (Picha na Huang Wanqing/Xinhua)

KIGALI - Kituo kidogo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua kimeanzishwa katika Taasisi ya Forever TVET iliyojengwa na kampuni ya China huko Kigali, Rwanda, ili kuhakikisha upatikanaji wa nishati thabiti na endelevu kwa chuo hicho.

Mradi huo unajumuisha uzalishaji umeme kwa nishati ya jua (PV), uhifadhi wa nishati, huduma ya kuchaji, na usimamizi wa kisasa wa nishati katika mfumo wa pamoja wa PV-Uhifadhi-Kuchaji-Vifaa, ukianzisha mfumo wa kisasa wa udhibiti wa nishati kwa matumizi yenye ufanisi wa juu na usambazaji kwa usahihi wa rasilimali za nishati.

Jitihada hiyo inalenga kuhimiza matumizi ya nishati safi, kuongeza ufanisi wa nishati shuleni, na kutoa jukwaa la kisasa la matumizi ya kihalisi kwa ajili ya elimu na utafiti.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi juzi Jumanne, Jenerali Cesar, mshauri mkuu wa ufundi wa Wizara ya Miundombinu ya Rwanda, amesema, mradi huo uliokamilika ni hatua kubwa ya safari ya pamoja ya kuelekea maendeleo ya kijani ya Rwanda, ushirikiano wa kielimu, na kuzidisha urafiki kati ya Rwanda na China.

"Tunaweka umuhimu mkubwa katika kupanua nishati safi, kuimarisha mfumo wetu wa elimu ya ufundi wa kazi, na kuongeza ushirikiano kati ya sekta ya umma na ya kibinafsi," amesema, akiongeza kuwa, "Mradi tunaousherehekea leo unaonesha malengo haya yote -- si tu ni chanzo cha nishati mbadala lakini pia ni kituo cha kutoa mafunzo na kufanya mazoezi kinachowawezesha vijana wetu kupata ujuzi muhimu wa kiufundi."

Gao Zhiqiang, konsuli wa mambo ya uchumi na biashara wa Ubalozi wa China nchini Rwanda, amesema kuwa tangu kuanzishwa kwake, Taasisi ya Forever TVET siku zote inafuata kanuni ya "mafungamano ya mafunzo na viwanda, na ustadi kwanza", ikifuatilia mahitaji ya maendeleo ya Rwanda huku ikiunganisha miradi yake na sekta muhimu kama vile mashine nzito, uhandisi wa umeme, na teknolojia ya upashanaji habari na mawasiliano.

"Katika miaka mingi iliyopita, imetoa mchango mkubwa katika kuhudumia kampuni na viwanda vya China, kuandaa vipaji wenyeji vya ufundi, na kuhimiza mawasiliano kati ya China na Rwanda katika utamaduni na elimu," amesema.

Wanafunzi wakiendesha kiigaji katika Taasisi ya Forever TVET iliyojengwa na China mjini Kigali, Rwanda, tarehe 8 Julai 2025. (Picha na Huang Wanqing/Xinhua)

Wanafunzi wakiendesha kiigaji katika Taasisi ya Forever TVET iliyojengwa na China mjini Kigali, Rwanda, tarehe 8 Julai 2025. (Picha na Huang Wanqing/Xinhua)

Mkufunzi akielezea kabineti ya kudhibiti umeme katika Taasisi ya Forever TVET iliyojengwa na China mjini Kigali, Rwanda, tarehe 8 Julai 2025. (Picha na Huang Wanqing/Xinhua)

Mkufunzi akielezea kabineti ya kudhibiti umeme katika Taasisi ya Forever TVET iliyojengwa na China mjini Kigali, Rwanda, tarehe 8 Julai 2025. (Picha na Huang Wanqing/Xinhua)

Picha iliyopigwa Julai 8, 2025 ikionyesha paneli za kuzalisha umeme kwa nishati ya jua katika Taasisi ya Forever TVET iliyojengwa na China mjini Kigali, Rwanda. (Picha na Huang Wanqing/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha