

Lugha Nyingine
China na Misri zapaswa kuwezesha biashara na uwekezaji wa pande mbili
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Misri Hanafy Ali Gebaly mjini Cairo, Misri, Julai 9, 2025. (Xinhua/Liu Bin)
CAIRO - China na Misri zinapaswa kuendelea kuwezesha biashara na uwekezaji wa pande mbili, kuimarisha kuwiana kiviwanda na muunganisho wa soko, na kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana kwenye kiwango cha juu zaidi, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema jana Jumatano mjini Cairo alipokutana na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Misri Hanafy Ali Gebaly.
Li yuko katika ziara ya kiserikali nchini Misiri kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mostafa Kamal Madbouly.
"Ingawa China na Misri ziko mbali kijiografia, urafiki kati ya nchi hizo mbili una historia ya muda mrefu," Li amesema.
Amesema, tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, haijalishi namna gani hali ya kimataifa inavyobadilika, urafiki wa jadi kati ya China na Misri haubadiliki, na uhusiano na ushirikiano wa pande mbili inaendelezwa vizuri, ikionyesha uhai mkubwa wa ndani, Li amesema
"China inapenda kuhimiza zaidi urafiki wa jadi na Misri, kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa, kuungana mkono kithabiti katika maslahi makuu na mambo makubwa yanayofuatiliwa ya kila upande, na kuhimiza uhusiano wa pande mbili kufikia kwenye ngazi mpya na kupata matokeo mapya zaidi katika ushirikiano wa pande mbili, ili kunufaisha vema watu wa nchi zote mbili" amesema.
Pia ametoa wito kwa pande zote mbili kudumisha mawasiliano ya kirafiki kati ya mabunge ya nchi hizo mbili, kuimarisha mawasiliano ya kisera na uzoefu kuhusu utawala wa nchi, na kuboresha zaidi maelewano.
Akisema kuwa China inapenda kuimarisha kuwiana kimaendeleo na Misri, Li amesema pande zote mbili zinapaswa kufanya ushirikiano wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kutumia Baraza la Ushirikiano kati ya China na nchi za Kiarabu na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika kuboresha ushirikiano wa pande mbili wa kiuchumi na kibiashara.
Kwa upande wake, Gebaly amesema kuwa Misri na China, kama nchi mbili zenye ustaarabu mkubwa wa kale, zina historia ndefu ya mawasiliano na urafiki wa kina kati ya watu wao.
"Misri inapongeza mafanikio ya ajabu ambayo China imepata katika maendeleo yake ya kiuchumi na kijamii, na inaamini kwa dhati kwamba chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping wa China, kwa mafanikio China itafikia maendeleo ya mambo ya kisasa ya China, na kuleta fursa mpya za ushirikiano kati ya China na nchi nyingine zinazoendelea," Gebaly amesema.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Misri Hanafy Ali Gebaly mjini Cairo, Misri, Julai 9, 2025. (Xinhua/Li Xiang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma