Mkutano wa AI Kuwezesha Maendeleo Bora ya Ustawishaji Vijijini wafanyika Nanning, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 11, 2025

Mkutano wa AI kuwezesha Maendeleo Bora ya Ustawishaji Vijijini, ulioandaliwa kwa pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Mipango na Uendelezaji Ustawishaji wa Vijiji ya Guangxi Guinong, Kituo cha Utafiti wa AI cha Akademia ya Sayansi ya Kilimo ya Guangxi, na Shirika la Kuhimiza Ustawishaji wa Kilimo na Viwanda Vijijini la Guangxi, umefanyika Jumanne wiki hii mjini Nanning, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi wa China.

Washiriki zaidi ya 300 kutoka mashirika ya kiserikali, taasisi za utafiti, mashirika ya kifedha na kampuni ongozi kutoka ndani na nje ya mkoa huo wa Guangxi walikusanyika pamoja kwenye mkutano huo wa Nanning, kuweka dira kwa mageuzi ya vijijini yanayowezeshwa na AI.

Wakati wa mkutano, miradi mbalimbali inayojikita katika ushirikiano, uwekezaji, na ufadhili wa AI, uhamishaji wa teknolojia na kadhalika ilitiwa saini, huku Jukwaa la Ushirikiano wa Kiviwanda wa Ustawishaji wa Vijiji la Guangxi likizinduliwa rasmi.

Imeelezwa kwenye mkutano huo kuwa, jukwaa hilo limejengwa kwa pamoja na taasisi za utafiti, mashirika ya kifedha na jumuiya za kijamii, likijikita katika kufungamanisha sera za kiviwanda za ustawishaji wa vijiji, teknolojia, fedha, masoko na mambo mengine ya rasilimali.

Wataalamu walioshiriki kwenye mkutano huo walikubaliana kuwa, kutumia AI kutatua tatizo la ufanisi wa kilimo na kujenga minyororo ya kisasa ya kilimo kwa bidhaa za kilimo zenye umaalumu kutakuja kuwa mafanikio muhimu katika mageuzi na kuboresha kilimo cha mkoa huo wa Guangxi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha