

Lugha Nyingine
China yapenda kuboresha biashara na kupanua ushirikiano na Misri
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Kamal Madbouly mjini Cairo, Misri, Julai 10, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)
CAIRO - Waziri Mkuu wa China Li Qiang alipokutana na mwenzake wa Misri Mostafa Kamal Madbouly mjini Cairo, mji mkuu wa Misri jana Alhamisi, amesema kwamba China inapenda kushirikiana na Misri ili kuboresha maendeleo ya biashara ya pande mbili na kuunda mambo muhimu zaidi ya ushirikiano vilevile mambo mapya ya kuleta ukuaji wa uchumi.
"Nchi hizi mbili zinaweza kupanua ushirikiano katika sekta zinazoibukia kama vile nishati mpya, magari yanayotumia umeme, akili mnemba na uchumi wa kidijitali," Li amesema, akiongeza kuwa China imekuwa ikiweka kipaumbele katika kuendeleza uhusiano kati yake na Misri katika sera yake ya diplomasia ya Mashariki ya Kati.
Amesema, mwaka 2024, China na Misri kwa pamoja zilisherehekea maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzisha ushirikiano wao wa kimkakati wa pande zote na mikutano miwili kati ya Rais Xi Jinping wa China na Rais Abdel Fattah El-Sisi wa Misri ilitoa mwongozo kwa ajili ya maendeleo ya siku za baadaye ya uhusiano wa pande mbili.
“Mwaka 2026, China na Misri zitaadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia. Katika hatua hii muhimu, China inapenda kudumisha mawasiliano ya karibu ya ngazi ya juu na Misri, kuimarisha mazungumzo ya kimkakati, kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa, na kuzidisha ushirikiano wa kivitendo” Li amesema.
Ametoa wito kwa pande zote mbili kuungana mkono katika njia ya ujenzi wa mambo ya kisasa na kuleta faida kubwa zaidi kwa watu wao.
"China inaiunga mkono Misri katika kuchukua jukumu kubwa zaidi katika mambo ya kimataifa na kikanda na inapenda kuratibu na kushirikiana kwa karibu na Misri ndani ya mifumo ya pande nyingi kama vile Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai kutekeleza ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, kulinda utandawazi wa uchumi na utaratibu wa kimataifa wa uchumi na biashara, kutetea maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea, na kuhimiza amani na utulivu katika Mashariki ya Kati na duniani.” amesema.
Kwa upande wake, Madbouly amesema kuwa Misri na China zimekuwa zikifurahia uhusiano wa muda mrefu na wa kina, huku urafiki wa jadi ukiwa umekita mizizi katika mioyo ya watu wao.
"Katika miaka ya hivi karibuni, chini ya uongozi wa wakuu wa nchi hizo mbili, ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya Misri na China umeonyesha msukumo mkubwa, na uko katika kipindi kizuri zaidi katika historia," amesema, akiongeza kuwa Misri inashikilia kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, inaheshimu mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya China, inaunga mkono kithabiti msimamo wa China juu ya suala la Taiwan ma masuala yanayohusiana na Xizang na Hong Kong na kithabiti inapinga kitendo chochote cha kuingilia kati mambo ya ndani ya China.
Baada ya mkutano huo, Li na Madbouly kwa pamoja walishuhudia utiaji saini nyaraka nyingi za ushirikiano katika maeneo kama vile biashara ya mtandaoni, maendeleo ya kijani na yenye kutoa kaboni chache, msaada wa maendeleo, mambo ya fedha na afya.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Kamal Madbouly mjini Cairo, Misri, Julai 10, 2025. (Xinhua/Liu Weibing)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma