

Lugha Nyingine
Kuondolewa silaha kwa PKK kunafungua "ukurasa mpya wa kihistoria" kwa Uturuki: Erdogan
Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki akizungumza kwenye Mkutano wa 32 wa Mashauriano na Tathmini katika Wilaya ya Kizilcahamam, Jimbo la Ankara, Uturuki, Julai 12, 2025 (Mustafa Kaya/kupitia Xinhua)
ANKARA - Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ametangaza kuwa Uturuki umefungua "ukurasa mpya" wa kihistoria, wakati Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi (PKK) kikianza mchakato wa kuondolewa silaha akisema: "Kufikia jana (Ijumaa), janga la kigaidi linaloendelea kwa muda wa miaka 47 limeingia katika hatua ya mwisho. Uturuki imeanza kufunga ukurasa mrefu, wa maumivu uliojaa machungu na machozi."
Siku ya Ijumaa wiki iliyopita, kundi la wanamgambo wa PKK lilichoma silaha zao katika jimbo la Sulaymaniyah, kaskazini mwa Iraq.
"Kuanzia sasa , tutakaa chini na kuzungumza -- siyo kwa silaha au vurugu, siyo kwa mgogoro, lakini kwa umoja, udugu, na mazungumzo ya ana kwa ana kwa kuondoa kikwazo cha ugaidi," Erdogan amesema wakati akihutubia wanachama wa Chama chake tawala cha Haki na Maendeleo katika wilaya ya Kizilcahamam, Jimbo la Ankara.
Shughuli hiyo ya kuondolewa silaha ilishirikiwa na wawakilishi kutoka Shirika la Taifa la Ujasusi la Uturuki, Serikali ya Mkoa wa Kurdistan, maafisa wa Iraqi, vikosi vya usalama, mashirika ya kiraia, na waandishi wa habari, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Anadolu la Uturuki.
Kundi hilo la PKK, ambalo limeorodheshwa kuwa kundi la kigaidi na Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya, limekuwa likipambana na serikali ya Uturuki kwa zaidi ya miongo minne.
Uturuki zinafanya operesheni za kijeshi mara kwa mara kulenga wanamgambo wa PKK kaskazini mwa Iraq, ambako kundi hilo lina maficho yake.
Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki akizungumza kwenye Mkutano wa 32 wa Mashauriano na Tathmini katika Wilaya ya Kizilcahamam, Jimbo la Ankara, Uturuki, Julai 12, 2025 (Mustafa Kaya/kupitia Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma