Semina ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Mauritania na China

(CRI Online) Julai 14, 2025

Shirikisho la Wanafunzi wa Mauritania waliosoma Vyuo Vikuu vya China limeandaa semina ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Semina hiyo imefanyika Jumamosi mwishoni mwa wiki katika mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott, ikiwa na kaulimbiu ya “Uhusiano na Matarajio ya Baadaye ya Ushirikiano wa Pamoja kati ya Mauritania na China,” na kukutanisha wasomi na wanasiasa, ambao walieleza historia na uhusiano wa pande mbili unaoendana na nyakati, na pia matarajio ya ushirikiano wa baadaye.

Rais wa Shirikisho hilo Yarbane Kharrachi amesema, maadhimisho hayo yanatoa fursa kubwa ya kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika kuunga mkono maendeleo endelevu na jumuishi.

Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Mauritania Tang Zhongdong amesema miongo sita iliyopita imeshuhudia ushirikiano mzuri kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali, na kutoa wito wa ujenzi wa jumuiya ya China na Mauritania yenye mustakabali wa pamoja kuwa mfano wa ushirikiano wa kunufaishana kati ya pande mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha