Afrika Kusini yataka kuimarisha uhusiano wa kibiashara na China kupitia maonyesho ya mnyororo wa ugavi

(CRI Online) Julai 14, 2025

Afrika Kusini inalenga kuimarisha uhusiano wake na China wakati ujumbe wake wa ngazi ya juu ukidhamiria kushiriki Maonyesho ya 3 ya Kimataifa ya Mnyororo wa Ugavi ya China.

Taarifa kutoka Ikulu ya Afrika Kusini imesema, Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Paul Mashatile, akiongozana na maofisa wa serikali, watahudhuria Maonyesho hayo yaliyopangwa kufanyika Beijing kuanzia tarehe 16 hadi 20 mwezi huu.

Taarifa hiyo imesema, ushiriki wa ujumbe huo wa ngazi ya juu ni fursa muhimu ya kuendeleza uhusiano wa ushirikiano wa kimkakati kati ya Afrika Kusini na China katika zama mpya.

Pia taarifa hiyo imesema, katika Maonyesho hayo, Afrika Kusini itatafuta kuboresha sekta za kimkakati kama nishati mpya, ugavi, madawa, madini, na uchumi wa kidijitali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha