

Lugha Nyingine
Simulizi za Miji | Ustaarabu katika Mtiririko: Maajabu ya wakati katika Mji wa Yinchuan, China
Katika jangwa lisilo na mipaka, moshi mpweke hupanda moja kwa moja; juu ya mto usio na mwisho, jua huzama likiwa na umbo la mviringo. Majangwa kwa kawaida hujulikana kama eneo lililokatazwa kwa maisha. Lakini katika Mji wa Yinchuan, Mji Mkuu wa Mkoa Unaojiendesha Kabila la Wahui wa Ningxia, kaskazini-magharibi mwa China, maisha huchanua kwa njia zisizotarajiwa.
Watu wa Tangut (Dangxiang) wa Enzi ya Xixia walijua sanaa ya utengenezaji divai miaka zaidi ya 800 iliyopita. Kijiji kando ya mto huko kinajulikana kwa ardhi zake oevu na vyanzo vingi vya maji ambavyo hurutubisha mizabibu, pamoja na mwanga wa jua na udongo wenye rutuba wa "eneo la dhahabu" kwa kilimo cha zabibu kwenye miinuko ya mashariki ya Mlima Helan.
Hifadhi ya taifa ya ardhioevu mjini Yinchuan pia ni makazi muhimu kwa ndege wanaohama hama.
Kama mji muhimu katika Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na dirisha muhimu kwa China kufungua kwa upande wa magharibi, chupa za mvinyo ziko tayari kuanza safari kuelekea kwenye meza duniani kupitia Mfumo wa Usafiri wa Muundo wa Reli na Bahari wa mji huo.
Yinchuan ni mji wa rangi zinazovutia: taa za yakuti kwenye skrini ambazo zinaangaza dunia; ngome kubwa za kahawia ambako filamu ya "A Chinese Odyssey" ilirekodiwa; karatasi nyekundu mikononi mwa fundi anayeunda sanaa ngumu ya mkasi; na picha ya kijani ya mfumo wa kukua pamoja kwa samaki na mipunga.
Usiku unapoingia, maisha ya mtaani ya Yinchuan hujaza uhai wa ujana. Beri za Goji, ambazo zilikuwa tiba za kale, sasa zinang'aa katika vikombe vya chai vinavyopendeza. Cheers, Yinchuan! Kwa historia iliyopita, na kwa nuru za siku za baadaye.
(Peng Yukai, Sheng Chuyi, Li Zheng, Alvaro Lago, Liang Hongxin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma