Kukarabati upya eneo la makazi kuboresha maisha ya wakazi wa Mji wa Fuzhou, China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 16, 2025
Kukarabati upya eneo la makazi kuboresha maisha ya wakazi wa Mji wa Fuzhou, China
Wakazi wakila chakula cha mchana kwenye kantini kwa wakazi wazee katika eneo la Cangxia Xincheng la Mji wa Fuzhou, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China, Julai 14, 2025. (Xinhua/Lin Shanchuan)

Katika miaka ya hivi karibuni, Mji wa Fuzhou wa Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China umekuwa ukifanya juhudi kubwa za kutekeleza mipango ya kujenga upya maeneo ya makazi ya hali duni ya mjini.

Cangxia Xincheng ni eneo lililokuwa bovu lenye mazingira mabaya mjini humo Fuzhou, hivi sasa limebadilika kuwa eneo la makazi yanayofaa kuishi kwa watu baada ya kufanyiwa ukarabati na ujenzi wa ngazi ya juu kwa zaidi ya mwaka mmoja kuanzia mwezi Julai mwaka 2000. Septemba 2021, mpango wa duru mpya wa kukarabati na kujenga upya ulitekelezwa katika mji huo, ukiwekwa mkazo katika kufungamanisha hali ya utamaduni na historia na urahisi wa maisha katika mji huo. Miundombinu ya huduma mahsusi imejengwa kama vile kantini kwa wazee na vituo vya kulelea watoto. Kupitia ukarabati huo wa maeneo ya wakazi wa mjini, maisha ya watu yameboreshwa sana. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha