Kutembelea tena jumba la ukumbusho wa makao makuu ya zamani ya Jeshi Jipya la Nne Anhui, China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 18, 2025
Kutembelea tena jumba la ukumbusho wa makao makuu ya zamani ya Jeshi Jipya la Nne Anhui, China
Picha ya Daraja la Ye Ting kwenye jumba la ukumbusho wa makao makuu ya Jeshi Jipya la Nne katika Wilaya ya Jingxian, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China. (Xinhua/Zhou Mu)

Jumba la ukumbusho wa makao makuu ya zamani ya Jeshi Jipya la Nne liko katika Tarafa ya Yunling ya Wilaya ya Jingxian katika Mji wa Xuancheng, Mkoa wa Anhui, China, eneo la jumba hilo ni la mita za mraba 20,000. Jeshi Jekundu la Nne lilikuwa moja kati ya majeshi ya kupigana vita na wavamizi wa China chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China.

Jumba hili ni moja ya maeneo muhimu ya urithi chini ya ulinzi wa serikali ya China, na lilijengwa kwenye msingi wa mabaki ya sehemu 11 za makao makuu ya zamani ya Jeshi Jipya la Nne yalikuwepo huko Yunling kutoka mwaka 1938 hadi 1941, wakati wa Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Wajapan.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha