Teknolojia ya Juncao yaunga mkono mpango wa kulisha watoto shuleni wa Rwanda (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 21, 2025
Teknolojia ya Juncao yaunga mkono mpango wa kulisha watoto shuleni wa Rwanda
Wakurufunzi wakitazama sampuli za uyoga kwenye Kituo cha Kielelezo cha Teknolojia ya Kilimo cha China na Rwanda katika Wilaya ya Huye, Rwanda, Julai 17, 2025. (Picha na Huang Wanqing/Xinhua)

KIGALI – Katika kusini mwa Rwanda, shule ya ufundi inakuza uyoga kwa kutumia teknolojia ya Juncao ili kuimarisha mpango wake wa kulisha wanafunzi, hali ambayo ni hatua ya kivumbuzi inayolenga kukabiliana na changamoto za muda mrefu za lishe kwa njia yenye gharama nafuu na endelevu.

Kulisha watoto shuleni kumekuwa sehemu muhimu ya sera ya elimu ya Rwanda, ikilenga kupunguza njaa ya watoto wakati wa saa za shule na kupanua ufikiaji wa kujifunza, hasa kwa watoto kutoka familia zenye kipato cha chini.

Katika Shule ya Ufundi ya Busasamana, mwalimu wa fizikia na mratibu wa kulisha watoto shuleni Alice Allouette Marie Munyurabanga anaona ulimaji uyoga kama njia yenye matumaini ya kuongeza ubora wa chakula kwa wanafunzi, akisema kwamba kilimo cha uyoga kinatoa fursa mpya za kuboresha milo inayotolewa na shule yake, hasa kwa wale ambao familia zao zinatatizika kifedha.

"Mpango wa kulisha watoto shuleni hukabiliwa na changamoto kubwa pale baadhi ya wazazi wanapokuwa hawawezi kumudu kulipa ada za shule kwa wakati. Kilimo cha uyoga kipekee kinaweza kuwa chaguo zuri la kuziba pengo hilo. Lakini hatuna maarifa na ujuzi wa kutosha kuhusu mbinu zinazohitajika kwa kulima uyoga." amesema.

Ameyasema hayo katika mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua wakati wa mafunzo ya teknolojia ya Juncao hivi karibuni kwenye Kituo cha Kielelezo cha Teknolojia ya Kilimo cha China na Rwanda (C-RATDC) katika Wilaya ya Huye, Mkoa wa Kusini wa nchi hiyo.

Munyurabanga ni miongoni mwa washiriki 57 kutoka nchi tano za Afrika waliohudhuria Warsha ya Pili ya Mafunzo ya Afrika juu ya Matumizi ya Teknolojia ya Juncao, iliyofanyika kuanzia Julai 16 hadi Julai 23.

Warsha hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Idara ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii, Wizara ya Kilimo na Rasilimali za Wanyama ya Rwanda na Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha Fujian nchini China, inazingatia katika matumizi ya teknolojia ya Juncao kwa kilimo cha uyoga, malisho ya mifugo na uhifadhi wa mazingira. Ilileta pamoja maafisa wa kilimo, waelimishaji na wataalam wa maendeleo kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Mapema mwezi Mei, Munyurabanga alishiriki kwenye ziara ya mafunzo nchini China, ambako alitambulishwa teknolojia ya Juncao kwa mara ya kwanza. Uzoefu huo, amesema, ulizua shauku mpya ya kutumia uvumbuzi huo katika shule yake.

Juncao, nyasi chotara iliyokuzwa katika miaka ya 1980 na Lin Zhanxi, profesa wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha Fujian, China ni teknolojia ya kilimo inayofanya kazi nyingi. Teknolojia hiyo hutumika zaidi kama vitu vyenye urutubisho vya kukuza uyoga wa chakula na dawa lakini pia hutumika kama malisho ya mifugo na kusaidia katika urejeshaji ikolojia. Uvumbuzi huo umeingizwa na nchi zaidi ya 100, ikiwemo Rwanda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha