Tamasha la kimtaifa la densi lafunguliwa katika Mkoa wa Xinjiang, China likiwa na maonyesho 52 (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 22, 2025
Tamasha la kimtaifa la densi lafunguliwa katika Mkoa wa Xinjiang, China likiwa na maonyesho 52
Wasanii wakifanya drama ya densi kwenye Tamasha la 7 la Kimataifa la Densi la Xinjiang China kwenye Ukumbi wa Umma wa Xinjiang mjini Urumqi, mji mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China, Julai 20, 2025. (Xinhua/Xin Yuewei)

URUMQI - Tamasha la 7 la Kimataifa la Densi la Xinjiang China limefunguliwa rasmi Jumapili mjini Urumqi, mji mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China, likishirikisha maonyesho 52 kwa muda wa siku 17 hadi Agosti 5, ambapo tamasha hilo linaleta pamoja vikundi 24 vya sanaa, vikiwemo kutoka nchi nane - Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Uzbekistan, Marekani, Italia, na Cambodia, vilevile vikundi 16 kutoka China.

Maonyesho kwenye tamasha hilo ni pamoja na drama ya dansi, opera, bale na densi za kisasa.

Aidha, Mji wa Urumqi unatumika kama ukumbi mkuu wa tamasha hilo, huku kukiwa na kumbi ndogo katika miji ya Ili, Hotan, Aksu, Karamay, Hami na Alaer.

Shughuli za tamasha hilo ni pamoja na Maonyesho ya Densi za Mtaa ya Njia ya Hariri ya Xinjiang 2025, maonyesho ya kijamii ya densi ya kijijini, kanivali ya kimataifa ya densi, na wiki ya opera ya kijadi.

Likiwa linaandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China, Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China, na serikali ya mkoa wa Xinjiang, Tamasha hilo limekuwa likifanyika tangu mwaka 2008, likivutia vikundi 138 vya sanaa kutoka nchi na maeneo zaidi ya 70 katika vipindi vyake sita vya awali na kutoa jukwaa muhimu kwa mawasiliano ya kiutamaduni chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha