Mandhari ya Mji wa Zhengzhou wa China, mwenyeji wa Mkutano wa Vyombo vya Habari na Washauri Bingwa wa SCO

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 23, 2025
Mandhari ya Mji wa Zhengzhou wa China, mwenyeji wa Mkutano wa Vyombo vya Habari na Washauri Bingwa wa SCO
Picha iliyopigwa tarehe 19 Julai 2025 ikionyesha Eneo la Kati la Biashara (CBD) katika Eneo Jipya la Zhengdong la Mji Zhengzhou, Mkoa wa Henan, katikati mwa China. (Xinhua/Li Jianan)

Mji wa Zhengzhou katika Mkoa wa Henan katikati mwa China unajulikana kuwa kituo cha kikanda cha uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, mji wa kihistoria na kiutamaduni wa kitaifa, na kituo cha usafirishaji jumuishi cha kimataifa.

Katika miaka ya hivi karibuni, mji huo Zhengzhou umefanya juhudi kubwa zaidi za kuhimiza maendeleo mazuri ya hali ya juu, kuongeza nguvu ya ushindani katika mambo yake ya jumla, na kujifungamanisha katika soko la nchi nzima. Kuanzia Julai 23 hadi 27, mji huo wa Zhengzhou utakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Vyombo vya Habari na Taasisi za Washauri Bingwa wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO).

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha