

Lugha Nyingine
Kazi za mikono za kijadi za ufumaji mazulia ya Kitibet zasukuma ustawi wa vijiji
![]() |
Mfanyakazi akitengeneza zulia la kitibet katika karakana ya Kundi la kampuni za mazulia la Shengyuan mjini Xining, Mkoa wa Qinghai, kaskazini-magharibi mwa China, Julai 21, 2025. (Xinhua/Qi Zhiyue) |
Kundi la kampuni za mazulia la Shengyuan liko katika Wilaya ya Chengzhong ya Mji wa Xining, Mkoa wa Qinghai, kaskazini-magharibi mwa China, likibobea katika kusanifu na kutengeneza mazulia za Kitibet. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007, Shengyuan imeajiri watu kutoka maeneo ya jirani, na 90% ya wafanyakazi wake wanatoka vijiji vya karibu, wakiwemo watu wa makabila ya Watibet na watu wa makabila mengine madogo madogo.
Zulia la Kitibet ni kazi ya mikono ya kijadi kwenye Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet yenye historia ya miaka zaidi ya 2,000. Nyuzi safi na sufu ya kondoo na ustadi maridadi wa kusuka na darizi zimefanya bidhaa hizo zinazotengenezwa kwa mikono kuwa maarufu na kukaribishwa sana na wateja wa ndani na nje ya China. Mwaka 2006, ujuzi wa ufumaji wa mazulia ya Kitibet kutoka Kijiji cha Jiaya cha Wilaya ya Huangzhong, Mkoa wa Qinghai, kaskazini-magharibi mwa China, uliorodheshwa kuwa mali ya kitaifa ya urithi wa utamaduni usioshikika wa China.
Katika miaka ya hivi karibuni, mkoa huo wa Qinghai umekuwa ukiongoza viwanda vya utengenezaji wa mazulia ya Kitibet kufungamanisha teknolojia ya kisasa na kazi za mikono za kijadi, ambayo inaingiza msukumo mpya katika ustawi wa vijiji wakati huohuo ikihifadhi ufundi na ustadi wa kijadi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma