Hafla ya kijadi yafanyika wakati wa kuwadia kipindi cha Dashu mjini Taizhou, Zhejiang, China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 23, 2025
Hafla ya kijadi yafanyika wakati wa kuwadia kipindi cha Dashu mjini Taizhou, Zhejiang, China
Meli ya uvuvi ikisafiri majini pamoja na mashua ya hafla kwenye hafla ya kijadi wakati wa kuwadia kwa kipindi cha Dashu katika kalenda ya kilimo ya China mjini Taizhou, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, Julai 22, 2025. (Xinhua/Weng Xinyang)

Watu katika maeneo ya pwani ya Mji wa Taizhou, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China walikusanyika jana Jumanne kufanya hafla ya kijadi katika wakati wa kuwadia kwa Kipindi cha Dashu, yaani kipindi cha Joto Kubwa, ambacho ni kipindi cha 12 katika vipindi 24 vya hali ya hewa vya kalenda ya Kilimo ya China. Watu hao walipanda mashua ya hafla yenye umbo la kijadi lenye nguzo tatu, wakiandama kupita vijiji halafu kuichoma mashua hiyo baada ya kuivuta kutoka kwenye bandari ya uvuvi. Mwaka 2021, hafla hiyo iliorodheshwa kuwa urithi wa utamaduni usioshikika wa China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha