

Lugha Nyingine
Trump atangaza makubaliano ya kibiashara baada ya kukutana na rais wa Ufilipino
WASHINGTON - Rais Donald Trump wa Marekani amekutana na mwenzake wa Ufilipino, Ferdinand Marcos Jr., jana Jumanne juu ya biashara na uhusiano wa pande mbili ambapo katika ujumbe wake kwenye mtandao wa Truth Social, jukwaa lake la mtandao wa kijamii baada ya mazungumzo yao, Trump amesema kuwa wamehitimisha Makubaliano ya Kibiashara, ambayo ndani yake Ufilipino itafungua soko kwa Marekani, na kutotoza Ushuru na kwamba Ufilipino italipa asilimia 19 ya ushuru.
Kwenye barua ya hivi karibuni kwa Rais Marcos, Trump alisema Marekani itaongeza ushuru kwa bidhaa za Ufilipino hadi asilimia 20 kuanzia Agosti 1.
Ikulu ya White House haijatoa maelezo zaidi kuhusu makubaliano hayo ya kibiashara na Ufilipino.
Marcos amesema uhusiano kati ya nchi hizo mbili "umekuwa ukipitia hadhi mbalimbali hadi kuwa uhusiano muhimu ambao inahitajika kuwa nao iwezekanavyo."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma