

Lugha Nyingine
Wataalamu wa Kimataifa wapongeza mafanikio ya China katika usimamizi wa tabianchi (2)
![]() |
Bronwyn Wake, mhariri mkuu wa jarida la Nature Climate Change, akizungumza kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Uongozi wa Tabianchi mjini Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Julai 22, 2025. (Taasisi ya Teknolojia ya Harbin/kupitia Xinhua) |
HARBIN - Licha ya kuwa ni ziara yake ya kwanza mjini Harbin, mji mkuu wa Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini kabisa mwa China, Bronwyn Wake, mhariri mkuu wa jarida la Nature Climate Change, ameshangazwa sana mara moja utaaluma wa wasomi wa China.
"China ina jumuiya imara ya wasomi walio na dhamira katika kusimamia mabadiliko ya tabianchi na kuelewa athari zake za kiuchumi," Wake amesema, akielezea matarajio yake kwa hekima zaidi ya China katika juhudi za ushirikiano wa kimataifa katika nyanja hizo.
Wake amekuja katika Chuo kikuu cha Teknolojia cha Harbin kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Uongozi wa Tabianchi, akiungana na wataalam kutoka nchi zikiwemo Uingereza na Hispania ambapo kwenye mkutano huo, walijadili masuala kama vile ushirikiano wa kimataifa wa tabianchi na uvumbuzi wa teknolojia zenye kutoa kaboni chache.
Wake amesema kuwa jarida la Nature Climate Change linachapisha maudhui ya mada mbalimbali, kama vile mfumo wa tabianchi, sayansi ya kibiolojia, mabadiliko ya tabianchi, na sera husika, ambazo watafiti wa China wamefanya tafiti nyingi nzuri.
Amesema kuwa wasomi wa China si tu wametafiti njia za kusukuma mbele usimamizi wa tabianchi ndani ya China lakini pia wametoa suluhu muhimu ambazo zinaboresha ushirikiano katika mabadiliko ya tabianchi duniani. Amesema, utafiti huo unaunda msingi wa sera bora za tabianchi zilizoratibiwa.
"China daima imekuwa ikibeba jukumu muhimu katika mazungumzo ya kimataifa ya tabianchi, kama vile Mkataba wa Paris," Wake amesema, akielezea matumaini kwamba China itaendelea kuchochea ajenda ya tabianchi duniani na kuunga mkono ushirikiano wa kimataifa.
Katika maoni ya Kannan Govindan, profesa katika Chuo Kikuu cha Adelaide nchini Australia, sekta ya nishati mbadala ya China inayostawi ni nguzo muhimu katika kuunga mkono hatua za tabianchi duniani.
Govindan amesema kuwa wakati hali mbaya ya hewa iliyokithiri inazidi kuvuruga uhakika wa minyororo ya usambazaji bidhaa duniani, teknolojia za nishati safi za China zinazozidi kupiga hatua kwa kasi -- kama vile paneli za jua, mitambo ya kuzalisha umeme kwa upepo, na mitambo ya kuzalisha umeme kwa maji -- si tu kwamba zinapunguza gharama za uzalishaji nishati duniani lakini pia zinaunga mkono maendeleo ya miundombinu katika nchi mbalimbali.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Taifa ya Nishati ya China, hadi mwisho wa Juni, uwezo uliofungwa wa China wa kuzalisha nishati ya upepo ulikuwa umefikia kilowati milioni 570, ongezeko la asilimia 22.7 kuliko mwaka jana wakati kama huo wakati uwezo wa nishati ya jua uliongezeka kwa asilimia 54.2 na kufikia kilowati bilioni 1.1.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma