

Lugha Nyingine
Miaka 25 ya upendo: Babu Mtibet alinda tumbili mwitu
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 25, 2025
LHASA - Kijiji cha Linze cha Wilaya ya Gongbo'Gyamda ya Mji wa Nyingchi, Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China ni makazi maarufu ya tumbili wa Kitibet, wanyama walio katika ulinzi wa daraja la pili la kitaifa nchini China. Tangu kuanza kazi ya kuwa mlinzi wa misitu katika mwaka 2000, Tobgye, babu mzee wa Kabila la Watibet, amekuwa akibeba kwa hiari jukumu la kulinda tumbili hao wa Kitibet wakati wa doria zake za milimani.
Upendo wake kwa tumbili umewagusa wanakijiji wa Kijiji hicho cha Linze, ambao husafisha sehemu ambayo mara nyingi tumbili hao hutokea, ili kuwaepusha kula takataka kimakosa.
Familia za tumbili hao wa Kitibet zinastawi, huku zaidi ya 7,000 kati yao wakiishi katika kijiji hicho kwa sasa.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma