Namna kampuni binafsi mkoani Guangdong inavyoongoza sekta ya vifaa vidogo ya umeme nyumbani ya China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 28, 2025
Namna kampuni binafsi mkoani Guangdong inavyoongoza sekta ya vifaa vidogo ya umeme nyumbani ya China
Mfanyakazi akifanya kazi kwenye mstari wa kuzalisha mashine za kutengeneza kahawa katika kiwanda cha Kampuni ya Vifaa vya Umeme vya Matumizi ya Nyumbani ya Xinbao huko Shunde, Foshan, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Julai 24, 2025. (Xinhua/Liu Dawei)

Katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2025, kiasi cha uagizaji na uuzaji nje bidhaa cha Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China kilifikia yuan trilioni 3.75 (dola za Kimarekani takriban bilioni 521), ikiongezeka kwa asilimia 4 kuliko mwaka 2024, na kupita kiwango cha nchi nzima kwa asilimia 1.5.

Katika miaka ya hivi karibuni, viwanda binafsi katika mkoa huo wa Guangdong vimekuwa vikifuata mwelekeo wa maendeleo ya kujipatia sifa bora zaidi wakati vikijitahidi kupanua uwepo wao katika masoko ya kimataifa.

Kampuni ya Vifaa vya Umeme Nyumbani ya Xinbao, yenye makao makuu yake huko Shunde mkoani humo, ni kiwanda kinachoongoza viwanda vya vifaa vidogo vya umeme vya matumizi ya nyumbani nchini China.

Kwa kila mashine 100 za kutengeneza kahawa zinazouzwa duniani kote, takriban 40 zinazalishwa na kiwanda hicho. Kiwanda hicho kinazalisha bidhaa mpya zaidi ya 1,000 kila mwaka, kikihusisha uwezo wake wa kuuza nje unaoendelea kukua na ahadi yake ya kufanya utafiti kwa kujitegemea na kufanya usanifu wa kivumbuzi. Mwaka 2024, kiwanda hicho cha kampuni ya Xinbao kilizalisha vyombo vidogo vya umeme vya matumizi ya nyumbani zaidi ya milioni 150, kikipata mapato kutoka biashara yake ya ng'ambo yanayozidi yuan bilioni 13 (dola za Kimarekani kama bilioni 1.81).

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha