ChinaVumbuzi | China yarusha kundi la satalaiti kwenye obiti ya urefu wa chini kiasi kutoka usawa wa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 31, 2025
ChinaVumbuzi | China yarusha kundi la satalaiti kwenye obiti ya urefu wa chini kiasi kutoka usawa wa Dunia
Roketi ya Long March-8A iliyobeba kundi la satalaiti kwenye obiti ya urefu wa chini kiasi kutoka usawa wa Dunia, ikirushwa kutoka eneo la kurushia vyombo vya anga ya juu vya kibiashara la Hainan katika Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Julai 30, 2025. (Xinhua/Zhang Liyun)

WENCHANG - China imefanikiwa kurusha kundi jipya la satalaiti kwenye obiti ya urefu wa chini kiasi kutoka usawa wa Dunia kutoka eneo la kurushia vyombo vya anga ya juu la Hainan katika mkoa wa kisiwa wa Hainan, kusini mwa China jana Jumatano, ambapo kundi hilo la satalaiti la sita la aina yake ambalo litaunda kundinyota la intaneti, limerushwa majira ya 9:49 alasiri (kwa saa za Beijing) likiwa ndani ya roketi ya kubeba ya Long March-8A.

Kundi hilo la satalaiti limeingia kwa mafanikio kwenye obiti iliyopangwa awali.

Urushaji huo unamaanisha safari ya 586 ya roketi za kubeba za mfululizo wa Long March. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha