Ding! Shubao na Jinzai wanakualika kwenye Michezo ya Dunia ya Chengdu! (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 31, 2025
Ding! Shubao na Jinzai wanakualika kwenye Michezo ya Dunia ya Chengdu!
Wateja wakiwa wamejaa kwenye duka la kuuza bidhaa rasmi za Michezo ya Dunia 2025 ya Chengdu. (People's Daily Online/Sun Shuyu)

Michezo ya Dunia 2025 ya Chengdu, ambayo itafanyika kuanzia Agosti 7 hadi 17, punde tu itawadia! Bidhaa mbalimbali za kuvutia za kiutamaduni na kibunifu zenye kujumuisha mambo ya maskoti za michezo hiyo – Shubao (“hazina ya Sichuan” katika lugha ya Kichina) na Jinzai (“Mtoto wa Chengdu” katika lugha ya Kichina) – zimeshika hisia za watu.

Zikiwa zimehamasishwa na panda pendwa na tumbili wepesi wa dhahabu wa Sichuan wenye pua fupi mtawalia, maskoti hizi zenye kuvutia zinaonesha moyo na uhai wa utamaduni wa Sichuan. Kuanzia midoli laini na mapambo ya sumaku ya kwenye friji, hadi beji na mabegi ya turubai, bidhaa hizi za aina mbalimbali zinachochea wimbi la manunuzi kwenye maduka ya bidhaa rasmi zilizoidhinishwa za michezo hiyo.

Zikiwa ni maskoti mbili zilizohamasishwa na wanyama hawa wawili adimu na alama wenye asili ya Chengdu, mji mkuu wa Mkoa wa Sichuan wa China, Shubao na Jinzai zinajumuisha kidhahiri maadili ya maendeleo ya kijani ya Chengdu. Kwa upole karimu wa Shubao na nishati ya ujana ya Jinzai, zinabeba shauku ya Michezo ya Dunia na kutoa mwaliko kwa dunia: Ungana nasi kwa ajili ya sherehe ya kimataifa ya michezo na urafiki!

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha