Mikoa ya Mashariki mwa China yaongeza juhudi za kuzuia maafa kutokana na kimbunga Co-May (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 31, 2025
Mikoa ya Mashariki mwa China yaongeza juhudi za kuzuia maafa kutokana na kimbunga Co-May
Waokoaji wakifanya kazi ya kutiririsha maji kutoka kwenye barabara iliyofurika maji mjini Ningbo, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, Julai 30, 2025. (Picha na Hu Xuejun/Xinhua)

Co-May, kimbunga cha nane mwaka huu kuikumba China, kimetua kwa mara ya pili katika Mji wa Shanghai, mashariki mwa China jana Jumatano alasiri baada ya kutua katika Mkoa wa Zhejiang mapema Jumatano asubuhi, kituo cha uangalizi wa hali ya hewa cha Shanghai kimesema.

Mikoa ya Zhejiang na Jiangsu imechukua hatua kuongeza juhudi za ukaguzi wa hatari na kuzuia maafa wakati huohuo ikiwahamisha wakaazi kutoka maeneo hatari. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha