Mtandao wa usafirishaji wachochea maendeleo katika Mkoa wa Xizang, China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 01, 2025
Mtandao wa usafirishaji wachochea maendeleo katika Mkoa wa Xizang, China
Picha hii iliyopigwa Aprili 1, 2024 ikionyesha barabara kuu ya kiwango cha juu kutoka Lhasa hadi Nyingchi katika Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini-magharibi mwa China. (Xinhua/Jigme Dorje)

LHASA - Kuanzia mwaka 2012 hadi 2024, Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini-magharibi mwa China umekamilisha uwekezaji wa jumla wa thamani ya yuan bilioni 401.925 (dola za kimarekani kama bilioni 55.86) katika mali zisizohamishika kwenye usafirishaji wa barabara kuu, na jumla ya urefu wa barabara kuu imeongezeka kutoka kilomita 65,200 mwaka 2012 hadi kilomita 124,900 ilipofikia mwishoni mwa mwaka 2024.

Mtandao wa usafirishaji wenye kiini chake katika Mji wa Lhasa na kupanuka kuelekea hadi miji ya Xigaze, Shannan, Nyingchi na Nagqu umeanzishwa, ambao unahimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kunufaisha watu wa makabila yote.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha