

Lugha Nyingine
Ghasia gerezani mashariki mwa Mexico yasababisha vifo vya watu 7 na wengine 11 kujeruhiwa
(CRI Online) Agosti 04, 2025
Sekretarieti ya Usalama wa Umma ya jimbo la Veracruz nchini Mexico imesema, wafungwa saba wameuawa na wengine 11 kujeruhiwa baada ya ghasia kutokea Jumamosi mchana katika gereza moja mjini Tuxpan, mashariki mwa nchi hiyo.
Askari wa Ulinzi wa Kitaifa, pamoja na wafanyakazi kutoka Idara ya Ulinzi ya Taifa na Sekretarieti hiyo, walidhibiti Kituo cha Urejeshwaji katika Jamii Jumapili asubuhi baada ya ghasia hiyo.
Pia Sekretarieti hiyo imesema, mioto kadhaa iliyosababishwa na vurugu hizo imezimwa na wafungwa kuhamishiwa katika gereza moja lililoko mjini Panuco.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma