Kiwango cha Ushuru wa Forodha cha Marekani chafika juu zaidi tangu mwaka 1934

(CRI Online) Agosti 04, 2025

Ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na Ofisi ya Bajeti ya Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani inaonyesha kwamba, pamoja na marekebisho zaidi ya sera za ushuru wa forodha za Marekani, wastani wa kiwango cha ushuru kinachofanya kazi umefikia 18.3%, ambacho ni kiwango cha juu zaidi tangu mwaka 1934.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa hatua mbalimbali za ushuru wa forodha zinazotekelezwa na serikali ya Marekani mwaka huu zitasababisha ongezeko la bei za bidhaa nchini Marekani kwa muda mfupi kwa asilimia 1.8, sawa na hasara ya wastani ya dola 2,400 kwa kila kaya.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa sera ya ushuru ina athari kubwa hasa kwa bei ya nguo na na viatu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha