

Lugha Nyingine
Idadi ya wahamiaji waliofariki kutokana na ajali ya boti yafikia 68
Idadi ya wahamiaji waliofariki baada ya boti waliyopanda kupinduka kwenye pwani ya Yemen imeongezeka na kufikia 68, huku wengine 74 hawajulikani walipo wakati juhudi za uokoaji zikiendelea.
Mkurugenzi wa Ofisi ya Afya katika mkoa wa Abyan, Abdul Qader Bajamil amesema, jana, timu za uokoaji zimepata miili 68 kando ya ufukwe kusini mwa mkoa huo, huku watu 12 wakiokolewa asubuhi ya siku hiyo.
Mamlaka za afya za mkoa huo zimethibitisha kuwa watu wote waliofariki na waliookolewa ni raia wa Ethiopia, na ni sehemu ya mfululizo wa wahamiaji kutoka Afrika wanaojaribu kwenda Yemen na hatimaye kusafiri kwenye nchi za Ghuba kutafuta fursa nzuri za kiuchumi.
Mamlaka za usalama za Yemen zimerejea tena wito wake kwa jamii ya kimataifa kushughulikia haraka chanzo cha uhamiaji usio rasmi na kuimarisha hatua za usalama baharini nchini humo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma