

Lugha Nyingine
AUSSOM yathibitisha kuwaua zaidi ya wapiganaji 50 wa al-Shabab kusini mwa Somalia
(CRI Online) Agosti 04, 2025
Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AUSSOM) imethibitisha Jumapili kuwa, wanajeshi wake wakiungwa mkono na vikosi vya serikali ya Somalia, wamewaua zaidi ya wapiganaji 50 wa al-Shabab wakati wa mapigano makali yaliyotokea Ijumaa mjini Bariire, kusini mwa Somalia.
Tume hiyo imefafanua kuwa, vikosi vyake vikishirikiana na jeshi la Somalia (SNAF), zilianzisha mashambulizi makubwa ya kuudhibiti tena mji wa Bariire tarehe 1 Agosti, ikijibu madai yaliyotolewa na al-Shabab kuhusu kuharibiwa kwa magari ya kivita ya Umoja wa Afrika na kurudi nyuma kwa wanajeshi wake baada ya mapigano makali huko Bariire.
Mji wa Bariire ambao ni maarufu kwa kilimo, ni moja ya maeneo ya kimkakati yaliyoko mkoa wa Lower Shabelle kando ya Mto Shabelle.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma