

Lugha Nyingine
Rais wa China atoa agizo muhimu juu ya kukusanya maoni na mapendekezo ya wanamtandao kuhusu kazi ya utungaji wa Mpango wa 15 wa miaka mitano
Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni ametoa agizo muhimu juu ya kukusanya na kutafiti maoni na mapendekezo ya wanamtandao wa Internet kuhusu kazi ya utungaji wa Mpango wa 15 wa miaka mitano wa China, akisisitiza kuwa shughuli ya kukusanya maoni na mapendekezo kuhusu kazi ya utungaji wa mpango huo kupitia mtandao wa Internet, iliyoshirikisha watu wengi, ni utekelezaji bora wa demokrasia ya umma katika mchakato kamili. Idara husika zinatakiwa kutafiti kwa makini maoni na mapendekezo yenye thamani kubwa yaliyotolewa na umma. Kamati za Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na serikali katika ngazi mbalimbali zinatakiwa kutoa kipaumbele kwa watu, kufanya uchunguzi kuhusu hali ya umma, kusikiliza sauti za umma, kukusanya busara za umma, ili kuunda nguvu kubwa ya pamoja ya kuendeleza juhudi za kuijenga China kuwa nchi ya mambo ya kisasa, na kuendelea kutimiza matarajio ya watu kwa maisha bora.
Shughuli ya kukusanya maoni na mapendekezo ya wanamtandao wa Internet kuhusu kazi ya utungaji wa Mpango wa 15 wa miaka mitano iliyofanyika kuanzia Mei 20 hadi Juni 20, imepokea jumbe milioni 3.11 kutoka wanamtandao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma