Viongozi wa kijeshi wa Uganda na Sudan Kusini wafanya mazungumzo kuhusu mvutano katika mpaka wa nchi hizo

(CRI Online) Agosti 05, 2025

Wakuu wa kijeshi kutoka Uganda na Sudan Kusini wamefanya majadiliano kufuatia mvutano mkali katika mpaka kati ya nchi hizo mbili.

Msemaji wa Jeshi la Uganda Felix Kulayigye amesema, naibu mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Uganda Sam Okiding na mkuu wa Jeshi la Sudan Kusini (SSPDF) Dau Aturjong Nyuol, walikutana Jumamosi katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba.

Kulayigye amesema, mazungumzo hayo ni sehemu ya juhudi za kidiplomasia zinazoendelea kukabiliana na mvutano katika mpaka na kuboresha ushirikiano wa pande mbili wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili.

Mkutano huo umefanyika siku chache baada ya mapigano makali kati ya askari wa Jeshi la Ulinzi la Uganda na Jeshi la Ulinzi la Sudan Kusini katika maeneo ya Fitina Mabaya na Goboro, yaliyoko kati ya wilaya ya Yumbe kaskazini magharibi mwa Uganda na kaunti ya Kajo-Keji ya nchini Sudan Kusini, na kusababisha vifo kwa pande zote mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha