

Lugha Nyingine
Afrika Kusini yasema kitendo cha Marekani kuongeza ushuru kitasababisha watu 30,000 kupoteza ajira
(CRI Online) Agosti 05, 2025
Wizara ya Biashara, Viwanda na Ushindani na Wizara ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano nchini Afrika Kusini zimesema, sera ya Marekani kuhusu kuongeza asilimia 30 ya ushuru kwa bidhaa za Afrika Kusini zinazouzwa Marekani itaathiri sana uchumi wa Afrika Kusini, huenda kusababisha watu 30,000 kupoteza ajira.
Katika mkutano wao na wanahabari uliofanyika jana, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Ushindani ya Afrika Kusini, Simphiwe Hamilton, amesema Marekani ni mshiriki wa tatu mkubwa wa biashara wa Afrika Kusini baada ya Umoja wa Ulaya na China, na kitendo cha kuongeza ushuru kitadhuru sana sekta ya utengenezaji wa magari na uboreshaji wa mazao ya kilimo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma