UNICEF yasema kusajili watoto wanaozaliwa ni muhimu katika kuendeleza haki za watoto wa Afrika

(CRI Online) Agosti 11, 2025

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limetoa maelekezo ya kisera huko Nairobi, likitoa wito wa kusajili watoto wachanga wanapozaliwa ili kuongeza ulinzi kwao na kuwawekea mustakabali mzuri zaidi.

Maelekezo hayo yametolewa wakati wa kuadhimisha Siku ya nane ya Usajili wa kiraia barani Afrika na Takwimu muhimu (CRVS), ambayo huwa tarehe 10 Agosti kila mwaka. Shirika hilo limesisitiza kwenye maelekezo hayo kuwa usajili wa uzazi ni haki ya msingi kwa kila mtoto. Lengo 16.9 la Malengo la Maendeleo Endelevu limetoa wito wa utoaji wa utambulisho wa kisheria kwa wote, lakini sasa takriban nusu ya idadi ya watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano wa Afrika kusini mwa Saharan hawajasajiliwa wakati walipozaliwa. Pia limeeleza kuwa Afrika inakadiriwa kuchangia theluthi moja ya watoto wote watakaozaliwa duniani ifikapo 2050, kwa hivyo usajili wakati wa kuzaliwa kwa wote ni sharti la lazima katika kulinda haki za watoto na pia hitaji la kidemografia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha