

Lugha Nyingine
Nigeria yashikilia msimamo wa kutowapokea waliofukuzwa Marekani
(CRI Online) Agosti 11, 2025
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Nigeria Bw. Kimiebi Ebienfa amesema Nigeria haitabadilisha msimamo wake dhidi ya kuwapokea watu waliofukuzwa kutoka Marekani, na kuongeza kuwa nchi hiyo kamwe haiwezi kukubali “mizigo ya ziada” kutokana na changamoto za kijamii na kiuchumi ilizo nazo.
Bw. Ebienfa amesema hakuna shinikizo lolote kutoka Marekani linaloweza kuishawishi Nigeria kubadilisha uamuzi wake kuhusu kupokea raia wa kigeni wanaofukuzwa kutoka Marekani, ambao baadhi yao wanatoka magerezani moja kwa moja.
Amesema hata kama nchi nyingine za Afrika zitakubali kupokea watu wanaofukuzwa kutoka Marekani, Nigeria haitakubali, kwani nayo ina changamoto zake.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma