

Lugha Nyingine
Umoja wa Afrika wasisitiza utaratibu wa kugawana raslimali kwa usawa ili kuwezesha jumuiya za asili za Afrika
Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Mahmoud Ali Youssouf amesisitiza haja ya kuendeleza utungaji wa sera za jumuishi na utaratibu wa kugawana raslimali kwa usawa ili kuziwezesha jumuiya za asili za Afrika.
Bw. Youssouf alitoa wito huo katika taarifa aliyoitoa jumamosi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya watu wa asili, ambayo hufanyika tarehe 9 Agosti kila mwaka. Siku hiyo inalenga kuongeza ufahamu kuhusu haki za watu wa kiasili duniani na kutambua mchango wao katika masuala muhimu ya kimataifa.
Akiangazia umuhimu wa kutambua urithi tajiri, mifumo ya maarifa, na uthabiti wa jumuiya za kiasili kote barani Afrika na sehemu nyingine, Bw. Youssouf alisisitiza umuhimu wa jamii hizo katika kuhifadhi tofauti za kitamaduni, kulinda mazingira, na kustawisha maendeleo endelevu kwa mujibu wa Agenda 2063, na mpango wa miaka 50 wa maendeleo ya bara la Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma