

Lugha Nyingine
Ghana yaomboleza waliokufa kwenye ajali ya helikopta
![]() |
Mtu huyu anaweka maua na kutoa heshima kwa wahanga wa ajali ya helikopta ya kijeshi huko Accra, Ghana, Agosti 9, 2025. (Picha imepigwa na Seth/Xinhua) |
ACCRA, Agosti 10 (Xinhua) – Jioni ya Jumamosi serikali ya Ghana ilifanya kumbukumbu ya maombolezo ya taifa ya siku tatu kutokana na vifo vya maofisa watano na wanajeshi watatu waliofariki katika ajali ya helikopta ya kijeshi Jumatano.
Maelfu ya watu wa Ghana, viongozi wa serikali, wabunge, na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa, akiwemo Rais wa zamani John Agyekum Kufuor na Makamu wa Rais wa zamani Mahamudu Bawumia, walishiriki kwenye maombolezo hayo yaliyofanyika mbele ya ukumbi wa Bunge mjini Accra.
Hotuba za maombolezo zilisomwa na taasisi na familia za watu wanane waliofariki huku kukiwa na sauti ya nyimbo za jadi za maombolezo zilizopigwa kwa filimbi, mwanga wa mishumaa ukitanda wakati wa jioni ya giza, zikiwa zimepangwa vyema kuonyesha hali ya maombolezo kwa taifa zima kutokana na tukio hilo la kusikitisha.
Rais wa Ghana John Dramani Mahama amelieleza tukio hilo kuwa ni msiba mkubwa kwa nchi, familia na ndugu wa marehemu. Helikopta ya kijeshi ilianguka katika Mkoa wa Ashanti nchini Ghana Jumatano, na kuwaua watu wote wanane waliokuwa ndani yake, wakiwemo Waziri wa Ulinzi Edward Kofi Omane Boamah, na Waziri wa Mazingira, Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi Ibrahim Murtala Muhammed.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma