

Lugha Nyingine
Mjumbe wa China asema jaribio la Israel la kutwaa mji wa Gaza lazima lipingwe vikali
Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Fu Cong (mbele katikati) akizungumza wikendi iliyopita katika mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Palestina na Israel, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Agosti 10, 2025. (Xinhua/Xie E)
UMOJA WA MATAIFA, Agosti 10 (Xinhua) -- Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Fu Cong, ameeleza wasiwasi wake mkubwa kuhusu mpango wa serikali ya Israel kuutwaa mji wa Gaza, na kusema jaribio lolote la kutwaa baadhi ya maeneo ya ardhi ya Palestina ni lazima lipingwe vikali.
Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Fu Cong, amesema kufuatia Baraza la Mawaziri la Usalama la Israel kupitisha mpango wa kuutwaa mji wa Gaza ni jambo linalotia wasiwasi mkubwa.
Akiongea kwenye mkutano wa dharura wa mwishoni mwa wiki kuhusu suala la Palestina na Israel uliofanywa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, balozi Fu ameitaka Israel ikomeshe mara moja hatua hiyo hatari.
Balozi Fu amesema, "Gaza ni mji wa watu wa Palestina, na ni sehemu muhimu ya ardhi ya Palestina. Hatua yoyote yenye lengo la kutaka kubadilisha muundo wake wa idadi ya watu na eneo, ni lazima ikataliwe na kukabiliwa na kupingwa vikali."
Balozi Fu amesema njia ya kijeshi sio njia nzuri ya kutatua mgogoro huo wa muda mrefu, na kusitisha mapigano mara moja ndio njia pekee sahihi ya kuokoa maisha na kuhakikisha kuachiliwa kwa mateka. Balozi Fu pia ametoa wito kwa serikali ya Israel kusikiliza sauti ya jumuiya ya kimataifa na watu wake, kukomesha mara moja mgogoro unaozidi kuongezeka, na kusitisha operesheni zake za kijeshi huko Gaza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma