

Lugha Nyingine
Wasimamizi wa amani Sudan Kusini waanzisha juhudi mpya za kufanikisha makubaliano ya amani
Wasimamizi wa amani nchini Sudan Kusini Jumatatu wametoa wito wa kuwepo kwa juhudi za pamoja miongoni mwa wadau wote wa nchi hiyo, ili kusaidia kufanikisha mpango wa amani.
Tume iliyoundwa upya ya ufuatiliaji na tathmini ya pamoja (RJMEC) ilitoa taarifa kwa ujumbe uliozuru kutoka Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AUPSC) mjini Juba, kuhusu hali ya kisiasa na usalama.
Tume hiyo imesema hali ya sasa nchini Sudan Kusini inahatarisha kurejea kwa vita ya muda mrefu ya kutumia silaha. Mkuu wa tume hiyo Bw. Berhanu Kebede ametoa wito kwa jitihada za pamoja za wadau wote kuhakikisha wanazihimiza pande za makubaliano ili kupanga njia ya kurejea kwenye amani ya kudumu.
Kwenye taarifa aliyoitoa baada ya mkutano wa Juba, Bw. Kabede amesema watu wa Sudan Kusini walioteseka kwa muda mrefu wanatamani amani na usalama wa kudumu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma