

Lugha Nyingine
Kundi la RSF la Sudan latuhumiwa kuwaua zaidi ya watu 40 mjini Darfur
Vikosi vya Msaada wa Haraka vya Sudan (RSF) vinaripotiwa kuwauwa zaidi ya raia 40 na kuwajeruhi makumi katika shambulizi lililofanywa kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao katika mji wa El Fasher, Kaskazini wa Darfur, siku ya Jumatatu.
Kamati ya Upinzani ya El Fasher, ambacho ni kikundi cha wanaharakati wanaopinga vita, imesema kwenye taarifa yake kuwa shambulizi lililofanywa kwenye kambi ya Abu Shouk lilijumuisha matumizi ya makombora na kuwaua watu majumbani. Kikundi kingine cha kujitolea kimeripoti kuwa takriban 40 wameuawa na wengine 19 wamejeruhiwa.
Shambulizi hilo limetokea wakati vikosi vya jeshi la Sudan (SAF) na makundi washirika, wanadai kuzuia shambulizi kubwa la ardhini lililofanywa na RSF katika mji huo, na kufanikiwa kulitia hasara kubwa kundi la RSF, kuwaua zaidi ya wapiganaji 200 wa kundi hilo na kuharibu au kukamata makumi ya magari ya kivita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma