

Lugha Nyingine
Baraza la Mawaziri la Guinea-Bissau laapishwa
(CRI Online) Agosti 12, 2025
Rais Umaro Sissoco Embalo wa Guinea-Bissau ameendesha hafla ya kuapishwa kwa awamu mpya ya Baraza la Mawaziri la nchi hiyo, litakaloongozwa na waziri mkuu Braima Camara, likiwa na mawaziri 26 na makatibu 11 wa kitaifa.
Kwenye hafla hiyo Rais Embalo ameitaka serikali mpya ishikamane, na kufanya vizuri maandalizi ya uchaguzi wa rais na wabunge utakaofanyika tarehe 23 Novemba. Aidha, ameahidi kupambana na ufisadi na uhalifu, na kuhakikisha uchaguzi unafanyika kama ulivyopangwa.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma