Somalia yathibitisha kuuawa kwa mkuu wa fedha wa kundi la al-Shabab

(CRI Online) Agosti 12, 2025

Wizara ya ulinzi ya Somalia imethibitisha kuwa kiongozi mkuu wa kundi la al-Shabab anayesimamia fedha ameuawa katika operesheni iliyofanyika Jumapili kwenye eneo la kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Wizara hiyo imesema mkuu wa fedha wa al-Shabab Abdullahi Abukar Ali aliyekuwa na jukumu la kusimamia kunyakua fedha kutoka raia na kuratibu uandikishaji wa askari watoto, aliuawa karibu na Hudur kwenye eneo la Bakool.

Wizara hiyo imesifu ushindi wa operesheni hiyo iliyofanywa na Jeshi la Somalia, ambalo lilisababisha kifo cha Abukar, ikisema operesheni hiyo yenye usahihi imeondoa tishio kubwa na imetoa pigo kubwa kwa mtandao wa utendaji wa kundi la al-Shabab katika eneo hilo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha