China na Marekani zatoa taarifa ya pamoja kufuatia mazungumzo yao ya kiuchumi na kibiashara ya Stockholm

(CRI Online) Agosti 12, 2025

China na Marekani zimetoa taarifa ya pamoja kufuatia mazungumzo yao ya kiuchumi na kibiashara mjini Stockholm. Kwa mujibu wa mazungumzo hayo mwakilishi wa China He Lifeng, Naibu Waziri Mkuu wa Baraza la Serikali, na wawakilishi wa Marekani Scott Bessent, Waziri wa Fedha, na Jamieson Greer, Mwakilishi wa Biashara wa Marekani, wamerejelea ahadi yao chini ya Taarifa ya Pamoja ya Geneva na kukubaliana kuchukua hatua ifikapo tarehe 12 Agosti 2025.

Hatua hizo ni kwamba Marekani iendelee kurekebisha matumizi ya kiwango cha ushuru wa ziada kwenye vifungu vya China, ikiwa ni pamoja na Hong Kong na Macao, viliyowekwa katika Agizo la Utendaji 14257 la Aprili 2, 2025, kwa kusitisha asilimia 24 ya kiwango hicho kwa muda wa ziada wa siku 90 kuanzia tarehe 12 Agosti, 2025, huku ikibakisha kiwango cha ushuru kilichosalia cha asilimia 10 kwenye vifungu hivyo kwa mujibu wa masharti ya Agizo hilo.

Pia China nayo kwanza itaendelea kurekebisha matumizi ya kiwango cha ushuru wa ziada kwenye vifungu vya Marekani kama ilivyobainishwa katika Tangazo la Tume ya Ushuru wa Forodha ya Baraza la Serikali Namba 4 la 2025, kwa kusitisha asilimia 24 ya kiwango hicho kwa muda wa ziada wa siku 90, kuanzia tarehe 12 Agosti, 2025, huku ikibakisha kiwango cha asilimia 10 kwenye vifungu hivyo. Na pili kupitisha au kudumisha hatua zote muhimu za usimamizi za kusitisha au kuondoa hatua za kujibu za ushuru zinazochukuliwa dhidi ya Marekani kama ilivyokubaliwa katika Taarifa ya Pamoja ya Geneva.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha