Kampuni ya Huawei ya China yazindua shindano la TEHAMA nchini Uganda kuwezesha vipaji vya ndani

(CRI Online) Agosti 12, 2025

Kampuni ya Huawei ya China imezindua shindano la kitaifa la teknolojia ya mawasiliano ya habari (ICT) 2025-2026 nchini Uganda ili kukuza vipaji vya ndani.

Kampuni hiyo imesema kwenye taarifa yake kuwa shindano hilo linalenga kuhimiza vipaji vya vijana kufanya vizuri kupitia mafunzo yaliyopangwa, kufahamishwa mambo ya TEHAMA, na mashindano, huku wakihimiza mabadiliko ya kidijitali.

Chini ya kauli mbiu ya "Connection, Glory, Future," shindano hilo linatarajiwa kuzileta pamoja taasisi za elimu ya juu, taasisi za mafunzo na wapenda teknolojia ili kusaidia kuhimiza mfumo wa ikolojia wa vipaji vya TEHAMA.

Akizindua mashindano hayo, Waziri wa Elimu na Michezo wa Uganda Bibi Janet Museveni, ameishukuru China na kampuni Huawei kwa kushirikiana na Uganda katika sekta ya TEHAMA, na kupongeza vijana wa Uganda wanaoshiriki katika programu za Huawei.

Balozi wa China nchini Uganda, Zhang Lizhong, ameipongeza kampuni ya Huawei kwa kujitolea kwake kwa mfumo wa ikolojia wa vipaji vya TEHAMA na mipango ya kampuni hiyo inayoziba pengo la ujuzi wa kidijitali nchini Uganda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha