Mashindano ya Uvumbuzi ya “Kilimo cha Kisasa (Kijiji cha Kidijitali)” yaanzishwa Guangxi, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 13, 2025

Hivi karibuni Mashindano ya Uvumbuzi ya "Kilimo cha Kisasa (Kijiji cha Kidijitali)" 2025 yameanzishwa mkoani Guangxi, China. Mashindano hayo yana kaulimbiu ya “Teknolojia ya Kisasa yaongeza uwezo wa wakulima na kuletea manufaa ”, yakifuatilia kilimo cha kisasa na ujenzi wa kijiji wa kidijitali.

Kazi kwa mashindano hayo zinapaswa kuhusu nyanja za kilimo cha kisasa (kijiji cha kidijitali), na kutekelezeka mkoani Guangxi au katika nchi za Asia ya Kusini-Mashariki. Mashindano hayo yanakaribisha zaidi mipango ya uvumbuzi kutoka kwa timu za wanafunzi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha