China na Misri zaanzisha mradi wa mafunzo ya ufugaji wa kuku kwa ajili ya wanawake wa Misri vijijini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 13, 2025
China na Misri zaanzisha mradi wa mafunzo ya ufugaji wa kuku kwa ajili ya wanawake wa Misri vijijini
Wanawake wakiwa kwenye mafunzo ya ufugaji kuku baada ya kufunguliwa kwa mradi wa mafunzo ya ufugaji kuku katika Jimbo la Menoufia, Misri, Agosti 11, 2025. (Xinhua/Sui Xiankai)

CAIRO, Agosti 12 (Xinhua) -- Ubalozi wa China nchini Misri, kwa ushirikiano na washirika wa ndani, wamezindua mradi wa mafunzo ya ufugaji wa kuku katika Jimbo la Menoufia nchini Misri ili kuwasaidia wanawake wa vijijini nchini humo kupata ujuzi wa kivitendo na kuongeza mapato ya kaya.

Mpango huo ambao umeandaliwa kwa pamoja na Muungano Kazi ya Maendeleo ya Kiraia wa Misri na Kampuni ya Kilimo ya New Hope Liuhe ya China, unashirikisha utaalam wa kilimo wa China katika usimamizi mzuri wa ufugaji wa kuku.

Meneja wa ufundi na daktari wa mifugo kwa kampuni ya New Hope Egypt Bibi Aya Abdeen, amesema mafunzo hayo yanahusu masuala muhimu ya ufugaji wa kuku, hasa kwa kuku wa Sasso, kuanzia wanapokuwa vifaranga wa siku moja hadi hatua ya kuuzwa sokoni.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha