Tanzania yazindua kampeni ya nchi nzima ya kukuza maeneo maalum ya kiuchumi

(CRI Online) Agosti 13, 2025

Serikali ya Tanzania imezindua rasmi kampeni ya kuhimiza uwekezaji katika nchi nzima inayolenga kuharakisha maendeleo ya maeneo maalum ya kiuchumi (SEZs), ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuiweka nchi hiyo kama nchi inayoongoza kwa viwanda na uwekezaji barani Afrika.

Waziri wa nchi ofisi wa rais anayeshughulikia mipango na uwekezaji Bw. Kitila Mkumbo, akizungumza katika hafla ya uzinduzi mjini Dar es Salaam, alisema kampeni hiyo inalenga kuunganisha maendeleo ya maeneo maalum ya kiuchumi na ukanda wa ukuaji wa taifa na miradi muhimu ya miundombinu.

Bw. Mkumbo amesema kampeni hii inaakisi dhamira yao thabiti kujenga uchumi imara wa viwanda na kuongeza kuwa maeneo maalum ya uchumi si maeneo maalum tu, bali pia ni msingi wa mkakati wao wa mabadiliko ya uchumi wa taifa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha